Translate

Jumatatu, 24 Agosti 2015

Jiko lisilo la moto/Kapu ,begi

Jiko lisilo tumia moto ni jiko linalohifadhi joto na kuendelea kupika chakula kwa mda mrefu kutokana na joto lililohifadhiwa  katika matirio ya kihami (insulate)kwenye ukuta wa kapu au begi.Sufuria ya chakula itapata joto kwenye jiko lolote kabla ya kuhamishiwa kwenye jiko lisilo la moto (kapu au begi).Jiko lisilo la moto si jiko geni katika bidhaa za kifuasi nishati, lipo ila uelewa wa jiko hili ni mdogo hasa katika wateja watumiaji majiko sanifu ya kisasa.
Jiko lisilo la moto ni kifuasi cha majiko aina zote kama jiko la umeme,jiko sanifu la mkaa,jiko la gesi na majiko mengineyo ya yaliyoendelezwa.

Jiko lisilo la moto linajulikana na limekuwwapo kwenye soko katika sehemu mbali mbali barani Afrika mfano  Tanzania linajulikana kama Jiko Kapu wakati Afrika kusini ni maarufu kama begi la ajabu (wonder bag). Jiko hili lisilo la moto limekuwa liki okoa matumizi ya nishati kwa sababu linapunguza matumizi ya nishati hasa kuni na mkaa kwa sababu auhitaji nishati nyingi  kupikia.

Baada ya kupika chakula  kwa kiwango  cha kawaida na  baadaye kuhamishia kwenye sufuria yenye joto kwenye jiko lisilo la moto kufanya chakula kiive taratibu.Epua sufuria ya chakula  ikiwa na joto nakuweka kwenye  kapu jiko  na kufunika na mfuniko vizuri vizuri joto la sufuria lisitoroke.Baada ya hapo chakula kitaendelea kuiva  taratibu kwa kiwango unachotaka kutokana na joto kwenye sufuria kuhamishiwa kwenye ukuta wa kihami (insulate)cha kapu na trei.Jiko hili rafiki wa mazingira linaokoa matumizi mengi ya mkaa na halitoi moshi hivyo ni bora kwa afya ya mtumiaji na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Ni jiko lisilotoa moshi rahisi ambalo ni salama,safi,madhubuti na rafiki wa mazingira linalohifadhi nishati na kusaidia kuhifadhi mazingira. Jiko lisilo la moto linaendelea kupika baada ya sufuria kuondolewa kwenye jiko la kawaida.

Faida
Jiko lisolo la moto lina okoa nishati kwa kutotumia kuni au mkaa mwingi. Jiko hili ni rahisi kutengeneza linahitaji kikapu na malighafi kama nguo kuukuu au material nyingine ambayo ni kihami (insulate) kama majani,mfano sponge zinazo kuja na vifaa vya umeme,
Linapunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 40%
Linapunguza moshi wa ndani (indoor air pollution) hivyo kuokoa afya ya mwanamke na mtoto.

Ni bei rahisi
 Linatumia malighafi ya kawaida na rahisi kutengeneza
Linapunguza matumizi ya maji kupikia kwa asilimia 25%.Maji yana baniwa tofauti na kuchemka,linahifadhi vimea,ladha ya chakula na maji ya kunywa.
Inasaidia kuhifadhi misitu ya asili na mazingira.
Jiko liliso la moto linaweza kutumika kuhifadhia chakula.
Linasaidia wanawake kutengeneza kipato katika fursa nyingine  kwa sababu hatumii muda mrefu kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.

Changamoto
Jiko halijulikani sana na watu wengi hawali tiili maanani

Jamii haina uelewa wa  vyanzo mbadala wa nishati baada ya mkaa na kuni