Translate

Jumatano, 23 Machi 2016

FANYA MWENYEWE MKAA WA BRIKITI 
Kwa mchanganyiko wa udongo wa ufinyanzi na chenga chenga za mkaa
MAHITAJI
-Vumbi au chengachenga za mkaa 80%
-Udongo bora wa ufinyanzi 20%
-Maji
MAELEKEZO YA UFANYAJI
-Changanya vumbi au chenga za mkaa na udongo wa ufinyanzi.Kiwango kinahitajika kuwa asilimia 80 chenga za mkaa na asilimia 20 za udongo.Changanya na maji mpaka upate mchanganyiko wa tope la mkaa.
-Baada ya hapo viringisha mchanganyiko huo ili upate tonge (pellet) la mkaa wa brikiti.
-Inashauriwa ukaushe vizuri kwa kuyaanika juani ili yakauke na kupata brikiti madhubuti.
UBORA WA MKAA BRIKITI
-Unaungua taratibu na kwa masaa 4 zaidi ya mkaa wa kawaida masaa 2.5
-Hautoi moshi
-Una joto madbubuti kwa kuoka
-Bei rahisi
-Unapunguza mkusanyiko wa hewa ya kabon monoksaidi



Jumamosi, 16 Januari 2016

Maelezo ya nembo KUNI AFRIKA (Kutokomeza Umaskini wa Nishati )

Muonekano wa nembo ya KUNI AFRIKA unaelezea athari  za umaskini wa nishati hasa kwa matumizi ya kuni na taa za mafuta ya taa kwa afya ya mama na mtoto jikoni.Shirika la Afya duniani WHO limeeleza uchafuzi wa hewa ndani  ya nyumba hasa jikoni umekuwa chanzo cha vifo vya mama na mtoto takribani milioni 4.3 kwa mwaka kuliko ukimwi,malaria na tb duniani.

Matumizi ya nishati kuni kupikia kwenye jiko la mafiga kuanzia asubuhi mpaka jioni ni sawa na kuvuta pakiti moja ya sigara. Matumizi ya nishati kuni yamekuwa yakichochea umaskini hasa unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke katika kutafuta kuni maporini.Hata kuuwawa kwa imani za kishirikina kutokana na macho yao kuwa mekundu hasa  kupikia nishati duni kama kuni na kinyesi cha ng’ombe jikoni.

Utumiaji wa kuni kama nishati umekuwa ukichangia katika ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu na kuchochea mabadiliko ya tabia nchi.

Kama Kuni Afrika tunajitolea  uelewa wa nishati jadidifu na upatikanaji wa bidhaa zake sokoni kupitia wasambazaji  wa bidhaa rafiki na ikologia Eco Footprints Tz ili kutokomeza umaskini wa nishati. Kuni Afrika ni kampeni ya kuhamasisha kutumia majiko sanifu na nishati mbadala ili kufuatilia Mpango wa upunguzaji hewa ukaa  katika kaya.

Uchomaji uzito uhai na  vichochezi ufu kama vyanzo vya nishati  kunaendeleza  kuharibu mazingira hiyvo hakuna budi kuelimisha jamii kuhusu nishati mbadala kama mkaa endelevu na vifuasi nishati kama jiko lisilotumia moto (fireless cooker),majiko sanifu ya kisasa (modern efficiently stove) kama eco zoom,envirofit,Bio lite cook stove, Cookswell Jiko etc.