Maelezo ya nembo KUNI AFRIKA (Kutokomeza Umaskini wa Nishati
)
Muonekano wa nembo ya KUNI AFRIKA unaelezea athari za umaskini wa nishati hasa kwa matumizi ya
kuni na taa za mafuta ya taa kwa afya ya mama na mtoto jikoni.Shirika la Afya
duniani WHO limeeleza uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba hasa jikoni umekuwa chanzo cha vifo
vya mama na mtoto takribani milioni 4.3 kwa mwaka kuliko ukimwi,malaria na tb
duniani.
Matumizi ya nishati kuni kupikia kwenye jiko la mafiga
kuanzia asubuhi mpaka jioni ni sawa na kuvuta pakiti moja ya sigara. Matumizi
ya nishati kuni yamekuwa yakichochea umaskini hasa unyanyasaji wa kijinsia kwa
mwanamke katika kutafuta kuni maporini.Hata kuuwawa kwa imani za kishirikina
kutokana na macho yao kuwa mekundu hasa kupikia nishati duni kama kuni na kinyesi cha
ng’ombe jikoni.
Utumiaji wa kuni kama nishati umekuwa ukichangia katika ukataji
miti ovyo na uharibifu wa misitu na kuchochea mabadiliko ya tabia nchi.
Kama Kuni Afrika tunajitolea uelewa wa nishati jadidifu na upatikanaji wa
bidhaa zake sokoni kupitia wasambazaji wa
bidhaa rafiki na ikologia Eco Footprints Tz ili kutokomeza umaskini wa nishati.
Kuni Afrika ni kampeni ya kuhamasisha kutumia majiko sanifu na nishati mbadala ili
kufuatilia Mpango wa upunguzaji hewa ukaa
katika kaya.
Uchomaji uzito uhai na
vichochezi ufu kama vyanzo vya nishati kunaendeleza kuharibu mazingira hiyvo hakuna budi kuelimisha
jamii kuhusu nishati mbadala kama mkaa endelevu na vifuasi nishati kama jiko
lisilotumia moto (fireless cooker),majiko sanifu ya kisasa (modern efficiently
stove) kama eco zoom,envirofit,Bio lite cook stove, Cookswell Jiko etc.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni