Translate

Jumamosi, 16 Januari 2016

Maelezo ya nembo KUNI AFRIKA (Kutokomeza Umaskini wa Nishati )

Muonekano wa nembo ya KUNI AFRIKA unaelezea athari  za umaskini wa nishati hasa kwa matumizi ya kuni na taa za mafuta ya taa kwa afya ya mama na mtoto jikoni.Shirika la Afya duniani WHO limeeleza uchafuzi wa hewa ndani  ya nyumba hasa jikoni umekuwa chanzo cha vifo vya mama na mtoto takribani milioni 4.3 kwa mwaka kuliko ukimwi,malaria na tb duniani.

Matumizi ya nishati kuni kupikia kwenye jiko la mafiga kuanzia asubuhi mpaka jioni ni sawa na kuvuta pakiti moja ya sigara. Matumizi ya nishati kuni yamekuwa yakichochea umaskini hasa unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke katika kutafuta kuni maporini.Hata kuuwawa kwa imani za kishirikina kutokana na macho yao kuwa mekundu hasa  kupikia nishati duni kama kuni na kinyesi cha ng’ombe jikoni.

Utumiaji wa kuni kama nishati umekuwa ukichangia katika ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu na kuchochea mabadiliko ya tabia nchi.

Kama Kuni Afrika tunajitolea  uelewa wa nishati jadidifu na upatikanaji wa bidhaa zake sokoni kupitia wasambazaji  wa bidhaa rafiki na ikologia Eco Footprints Tz ili kutokomeza umaskini wa nishati. Kuni Afrika ni kampeni ya kuhamasisha kutumia majiko sanifu na nishati mbadala ili kufuatilia Mpango wa upunguzaji hewa ukaa  katika kaya.

Uchomaji uzito uhai na  vichochezi ufu kama vyanzo vya nishati  kunaendeleza  kuharibu mazingira hiyvo hakuna budi kuelimisha jamii kuhusu nishati mbadala kama mkaa endelevu na vifuasi nishati kama jiko lisilotumia moto (fireless cooker),majiko sanifu ya kisasa (modern efficiently stove) kama eco zoom,envirofit,Bio lite cook stove, Cookswell Jiko etc.