Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi wa Misitu Afrika Mashariki
Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha
mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na
MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga unachochewa na shughuli za binadamu hasa uharibifu wa misitu
(deforestation) na kukata miti ovyo
(forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama
nishati ya kaya.
Utengenezaji wa mkaa
kwa tanuru la udongo usio madhubuti umekuwa chanzo cha kiwango kikubwa cha hewa ukaa inayopotea
katika kitendo cha kukabonisha (carbonization) na kupata mkaa kidogo kulingana
na kuni zilizoyotumika. Nchini Kenya kampuni ya siku nyingi ya bidhaa za kuhifadhi nishati
Cookswell Jiko wameboresha na kutengeneza
tanuru la pipa la bati kwa kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti
ovyo na uharibifu wa misitu.
Tanuru hili la pipa madhubuti liloboreshwa na kusanifiwa Kenya na wasanii wa
Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya nazi,magunzi ya mahindi na mianzi
ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha
ni mkombozi wa misitu na miti kwa sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa
kwa tanuru la udongo, bali kutumia matawi yaliyopogolewa vizuri na kutengeneza
mkaa mwenyewe (DIY).
Kwa kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa
misitu na kupunguza hewa ukaa na kufanya
Mkaa kuwa Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati
kutoka Cookswell Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la
kuikarisha (barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book
@Cookswell saving jiko.
Tanuru hili la pipa
linapatikana pia Tanzania kwa wasambazaji wa bidhaa rafiki mazingira na
nishati jadidifu Eco Footprints Tz na mradi wa kutokomeza umaskini wa nishati
KUNI AFRIKA.
OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU