TENGENEZA MWENYEWE
BALBU CHUPA YA JUA
Balbu chupa ya jua ni
balbu inayotokana na chupa ya maji iliyotupwa
kama taka kwa kujaza maji pamoja na jiki (bleach) ili kupata mchanganyiko ndani ya chupa unao
pindisha (refraction) miale ya jua. Balbu chupa ya jua yenye mchanganyiko wa maji na
jiki (bleach) , inatakiwa nusu chupa upande wa mdomo kuwa nje ya bati na kitako
cha chupa kuwa ndani. Hivyo maji yenye mchanganyiko wa jiki (bleach) hupindisha
miale ya jua na kufanya eneo lenye giza kupata mwanga huo wa kati wa mchana
hasa katika nyumba za makazi msongamano.
Usanifu huu wa balbu chupa ya jua (solar bottle bulb) umewezesha
kupunguza umaskini wa nishati ya mwanga kwa nyumba ambazo hazipati mwanga safi
wakati wa mchana kutokana na kutokuwa na
uwezo wa kuunganishiwa umeme wa gridi ya taifa. Usanifu huu umeweza kuwa rahisi
kutokana na upatikanaji wa rasilimali hasa chupa zilizotupwa kama uchafu ambazo
huchukua zaidi ya miaka mia tano kuoza
hivyo kuzorotesha afya ya mazingira.Pia usanifu huu wa balbu chupa ya umeme jua
umesaidia katika mrudisho na matumizi rafiki na mazingira.
MAHITAJI
Chupa ya maji iliyoisha matumizi yake hasa ya lita 1
Jiki (bleach) ya kufulia nguo
Maji safi
Kipande cha bati inchi 9 kwa 10
JINSI YA KUUNGA
Kata mzingo saizi ya kipenyo cha chupa kwenye kipande cha bati 9 kwa 10
Mzunguko wa mzingo ukatwe vizuri ili kufanya chupa ifiti kwa
uthabiti
Kata kipande cha mpira cha saizi ya mzunguko ili kusaidia
chupa kushika vizuri ikisaidiwa na gundi.
Jaza maji safi kwenye chupa ya lita moja
Weka kiwango cha kifuniko kimoja cha jiki kwenye kwenye chupa
ya maji lita moja kupata mchanganyiko wa maji na jiki na funga vizuri kwa
kupakalia na gundi.
Baada ya hapo fitisha chupa hiyo ya mchanganyiko kwenye
kipande cha bati cha inchi 9 kwa 10 kwa kupakalia gundi ya plastiki pamoja na
mzunguko wa kipande cha mpira.
Kata bati la paa ya nyumba saizi ya uwazi mdogo wa 7 kwa 8
ili kupachika kipande cha bati 9 kwa 10 chenye chupa balbu kwenye paa la
nyumba.
Paka gundi ya bati upande wa juu pembezoni ya uwazi wa bati 7
kwa 8 ili kufitisha kipande cha bati cha
8 kwa 10 chenye balbu chupa ya umeme jua
Baada ya hapo utakuwa tayari umefutisha kipande cha bati
kwenye paa la nyumba na kuwa tayari kupata mwanga wa balbu jua kupitia chanzo
cha nishati ya jua.
FAIDA YA CHUPA BALBU YA UMEME JUA
Balbu chupa ya jua ina uwezo wa kutoa mwanga wa wati 55 wa
kati wa mchana jua likiwaka
Rafiki wa mazingira kutokana na mrudisho kwenye matumizi ya
chupa tupu ya plastiki baada ya kuisha matumizi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni