Historia ya Jiko banifu/Sanifu KCJ
Historia ya jiko
sanifu barani Afrika inaanzia miaka ya 1970 na kuendelea mpaka miaka ya
1980.Tokea mwaka 1982 Shirika la Nishati na Mazingira Kenya KENGO lilifanya
tafiti ikishirikiana na wataalamu wasomi mmojawapo ni Dr Maxwell Kinyanjui
kufanya tafiti na kuendeleza matumizi ya jiko la ufinyanzi.Jiko hili lina
chimbuko kutoka Thailand ambako lilianzia kutokana na jiko ‘ndoo’.Taasisi kama
CARE,UNICEF na Bellerive zimefanya kazi kubwa kutoa mchango wa kifedha na
kuwezesha kuendeleza jiko na namna ya kulitengeneza pamoja na mashirika ya
misaada kama Marekani (USAID),Ujerumani (GTZ) na mashirika mengineyo. Mtaalamu,msanifu
na msomi Dr Maxwell Miringu Kinyanjui kutoka Kenya alifanikisha maendeleo ya jiko hili kuwa
sanifu na bora kwa matumizi ya nishati
ndogo ya mkaa.Kutokana na tafiti,fafanuzi na biashsra ikafanya jiko sanifu (ufinyanzi) kutambulika kama jiko la
kupunguza matumizi ya nishati ya kupikia
mkaa Kenya.Kwa mara ya kwanza jiko kwenda sokoni lilikuwa linauzwa bei ghali
kutokana na watumiaji wengi baadhi yao kuwa ni maskini wanaotumia jiko la
mafiga matatu. Baada ya kufikiriwa kwa makini hitimisho lilifikiwa na wataalamu
kwamba kutokana na jiko ni geni sokoni basi lisi wekewe ruzuku ili liende
sokoni lishindane kama bidhaa nyingine na kuleta ushindani thabiti. Mwanzo jiko
Sanifu (ufinyanzi) lilikuwa ghali,mauzo yalikuwa taratibu na ubora
ulitofautiana kutokana na kuigwa utengenezaji na wasanifu wengine bila kufuata
vigezo kuwa na majiko sanifu feki yasiyo na ubora kama ulio kusudiwa.Kuendelea kuongezeka kwa watengenezaji na wauzaji wa
majiko sanifu kukaongeza ushindani na hii ikaongeza uvumbuzi wa kutengeneza
chaga za jiko kwa kutumia udongo ufinyanzi pamoja na simenti ili kupata chaga
bora itakayo akisi joto na kukaa nalo muda mrefu.
Sehemu ya jiko
Jiko sanifu au
jiko banifu lina chaga ambayo ndio
inayobeba mkaa wa moto na kuhifadhi
kutunza kwenye chaga amabayo imetengenezwa kwa udongo wa ufinyanzi ulio na
uwezo wakuhifadhi joto. Hivi sasa chaga zinaboreshwa kwa udongo ufinyanzi unachanganywa na simenti kufanya chaga iwe ngumu na isiharibike
mapema.Baadhi ya wasanifu na mafundi majiko wanaoiga jiko hili wamekuwa
wakitengeneza chaga zisizo na ubora ulio kusudiwa. Baadhi ya watengenezaji wa
majiko haya barani Afrika kama Cookswell Jiko Kenya na Tatedo Tanzania
wanashauri chaga bora ni zile zenye
kudumu mda mrefu na uwezo wa kuhifadhi joto lisipotee kuonyesha uendelevu. Jiko
hili Sanifu limechangia kukua ujasiriamali kwa
watengenezaji wa majiko ya kawaida ya bati sasa hivi wanatengeneza fremu ya jiko na chagga baada ya jiko hili
kuwa maarufu katika kaya za Afrika Mashariki.
Kusambaa kuingia
Tanzania
Jiko hili sanifu
liliingia Tanzania miaka ya 1990 kutokea Kenya pale Shirika la Nishati Asili na
Jadidifu Tanzania TATEDO kupata mafunzo kutoka kwa msanifu na muendelezaji jiko hili barani Afrika Dr Maxwell Kinyanjui. Tatedo
walikuwa wa kwanza kueneza matumizi ya
jiko hili na kuwezesha wajasiriamali wa nishati jadidifu ili kutumia jiko hili
katika kaya za Tanzania.Mtaalamu wa Cookswell Jiko Teddy Kinyanjui anasema ili bidhaa ya jiko sanifu iweze
kupenya sokoni inahitaji miaka 10 mpaka 20.Kwa hiyo kwa jiko sanifu (ufinyanzi)
KCJ mpaka kufikia mwaka 2002 jiko sanifu lilikuwa limepenya soko la Tanzania na
mpaka kufikia mwaka 2012 jiko hili lilikuwa linajulikana na maarufu kama jiko
banifu,bora au sanifu. TATEDO wameendelea kupanua aina ya bidhaa hii ya jiko
sanifu kwa kutengeneza aina mbalimabali za jiko hili kukidhi mahitaji ya wateja mbali mbali kama Sazawa.
Faida ya Jiko
sanifu
Yana punguza
matumizi ya kichochezi nishati (mkaa) kwa asilimi sabini na moja 71%.
Hayachochei uzalishaji wa moshi hewa ukaa (carbon).
Yana usalama wa
joto na bati kutokana na joto kuhifadhiwa katika chaga bila kutorokea kwenye
bati
Kumeongeza ajira
kwa watengenezaji na ujasiriamali kwa viwanda vidogo vya kutengeneza chaga za
ufinyanzi
Yanahifadhi
nishati kwenye chaga
Yana dumu muda
mrefu
Uzoefu
unaonyesha yanapunguza gharama ya matumizi ya mkaa kwa asilimia hamsini 50%
Jiko Sanifu na Mkaa
Jiko hili
linategemea mkaa unaotokana na mti ili kuchochea na kuhifadhi joto kwa matumizi
ya kupikia.Kumekuwa na dhana potofu kwamba mkaa unatumika na maskini tu na
hauna faida yoyote katika jamii au ni ‘nuksi’ katika uhifadhi wa misitu ya
asili.Inashauriwa kupanda miti ilikuendelea kupata bidhaa ya mkaa inyotumika
katika majiko banifu.Mkaa ni nishati jadidifu kama miti itakuwa inapandwa kwa
ajili ya bidhaa mkaa.Pia kila mwananchi kupanda mti katika eneo lake analoishi
ili kutengeneza mkaa wake mwenyewe (DIY) kwa kukabonisha matawi ya miti,magunzi mapute ya nazi na kupata
mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).
Imeandikwa na
Mckene Ngoroma kwa msaada wa vyanzo vya taarifa Teddy Kinyanjui wa COOKSWELL JIKO KENYA na TATEDO Tanzania