Matembezi na Kuokota WALK &PICK SINZA-TANDALE-MAGOMENI
26 OCTOBA 2014
Tembea na okota ni mpango wa kufanya jiji la Dar es salaam kuwa safi mpaka kufika mwaka 2020 (clean Dar by 2020) mpango huu wa
kutembea na kuokota taka unfanyika kila jumapili ya mwisho wa mwezi katika
mitaa ya jiji la Dar es salaam. Mpango huu ni wakipekee katika aina za matembezi
amabayo nimekuwa nikijitokeza jiini Dar
es Salaam. Katika kupinga utupaji taka ovyo wa jamii katika maeneo ya jumuiya
na makaazi na kufikia malengo ya kuwa na jiji safi mpaka kufika mwaka 2020
(CLEAN DAR BY 2020). Tembea na okota au walk and pick ni matembezi
yaliyoanzishwa na organization inayoitwa Voice Giving iliyoko Kinondoni .
Kwa
mpango huu uliobuniwa na vijana wa Voice Giving uko sambamba na shindano la WWF Earth Hour City Challeng ambao umeingiza Dar
es Salaam kushindania kuwa jiji safi na kupunguza hewa ukaa kwa kutumia nishati jadidifu
na kupanda miti. Ushirikishi wa jamii
katika matatizo yao mfano kutoa elimu kwa wakazi na kuonyesha mfano kwa kufanya
usafi wa mazingira na makaazi yetu pamoja na utupaji wa taka za platik sehemu zisizosahihi.Takataka
zimekuwa zikizorotesha afya ya mazingira
hasa plastiki ambayo inachukua miaka 1000 kuoza na kuleta athari mbali mbali katika viumbe
hai nchi kavu na baharini.Tembezi la tarehe
26 octoba ni tembezi lililonipa changamoto
ya kufikiria kwa upana tatizo na
suluhisho la kukabiliana na taka taka katika jiji la Dar es Salaam. Tembea na
okota (walk and pick) ni moja ya matembezi ya harakati amabalo nimepata uelewa na elimu ya kutosha kama
mjasirianali wa mazingira pamoja na kijamii kuhusu taka taka za Dar es salaam.Kuanzia
Sinza kijiweni mpaka Shule ya Msingi Magomeni ni elimu niliyoipata katika
uchafuzi wa mazingira na tabia za watu wa Dar es salaam katika muono wa taka
taka.Kuchelewa kufika kwa halmashauri au watoa huduma ya taka kituoni na kukuta
taka zimefurika huku ziki hatarisha afya za wakazi hasa kituo cha pili mtaa wa
Tandale uzuri barabarani tulikuta lundo la takataka karibu namazingira wanayo
cheza watoto.
Katika tembezi hili takataka nyingi mitaani ni plastic material
pamoja na karatasi na maboksi ambayo ni rahisi kurudishwa.Ni baadhi ya maskini
wa mijini wanajua habari ya mazingira na kutotupa taka ovyo mfano kuanzia sinza
kijiweni mpaka darajani kuingia kata ya Tandale ina taka nyingi zikiwemo
plastic za viroba.Mitaro ya maji machafu ndipo taka zilipo tulia ampapo wakazi
wanachukulia urahisi huo huku wakisubiri mvua zinyeshe ziweze kusukumiwa maeneo ya baharini.Taka nyingi ambazo ziko
barabarani zinaweza kutokomezwa ikiwa abiria na wenye mabasi kupitia vyama vyao
kama DAROBA wata shurutishwa kufuata sharia zilizowekwa tutaweza kutokomeza
uchafuzi huu. Sisi wakaazi ndio wazalishaji wa taka taka hasa katika matumizi
yetu ya kila siku kufanikisha mahitaji yetu.Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi au
kutupa taka sehemu sahihi baada ya
matumizi ya bidhaa zenye vifungashio vya mifuko ya plastiki au kukataa kabisa
kufungiwa bidhaa na mifuko ya plastiki. Kila raia awe mhamasishaji wa kutotupa
taka ovyo mfano kama mji wa Moshi kila raia anaogopa kutupa taka ovyo kutokana
na sherika kali ya kutozwa faini shilingi elefu hamsini
hapa managing director wa Eco footprint tz akitembea na kuokota taka
Hapa MD wa Eco footprints Tz akitoa elimu ya mazingira
kazi nzuri
JibuFutaShukrani Suavity products tunaleta mabadiliko kwenye mitaa yetu, let keep #zerowaste
JibuFutaNaamini kwa pamoja tuta enzi asili yetu na mm ninatengeneze chaga za majiko nomba tuwasiliane kama mtakua na uhitaji 0654343308
JibuFuta