Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi wa Misitu nchini Kenya
Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha
mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na
MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga unachochewa na shughuli za binadamu hasa uharibifu wa misitu
(deforestation) na kukata miti ovyo
(forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama
nishati ya majumbani.Utengenezaji huu wa mkaa kwa tanuru la udongo usio
madhubuti umekuwa chanzo cha kiwango
kikubwa cha hewa ukaa inayopotea katika kitendo cha kukabonisha (carbonization)
na kupata mkaa kidogo kulingana na kuni zilizoyotumika.
Nchini Kenya kampuni ya
bidhaa za kuhifadhi nishati Cookswell Jiko wameboresha na kutengeneza tanuru la pipa la bati kwa
kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti ovyo na uharibifu wa misitu.Tanuru
hili la pipa madhubuti liloboreshwa na
kusanifiwa Kenya na wasanii wa Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya
nazi,magunzi ya mahindi na mianzi ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco
charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha ni mkombozi wa misitu na miti kwa
sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa kwa tanuru la udongo, bali
kutumia matawi yaliyobanguliwa vizuri na kutengeneza mkaa mwenyewe (DIY).
Kwa
kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa misitu na kupunguza hewa ukaa na kufanya Mkaa kuwa
Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati kutoka Cookswell
Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la kuikarisha
(barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book na tovuti yao.
Tanuru hili la pipa
linapatikana Tanzania kupitia Eco Footprints Tz.
Tanuri la pipa la chuma Cookswell Jiko lililoboreshwa. OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU
Imeandikwa na Mckene Ngoroma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni