Translate

Jumatano, 23 Machi 2016

FANYA MWENYEWE MKAA WA BRIKITI 
Kwa mchanganyiko wa udongo wa ufinyanzi na chenga chenga za mkaa
MAHITAJI
-Vumbi au chengachenga za mkaa 80%
-Udongo bora wa ufinyanzi 20%
-Maji
MAELEKEZO YA UFANYAJI
-Changanya vumbi au chenga za mkaa na udongo wa ufinyanzi.Kiwango kinahitajika kuwa asilimia 80 chenga za mkaa na asilimia 20 za udongo.Changanya na maji mpaka upate mchanganyiko wa tope la mkaa.
-Baada ya hapo viringisha mchanganyiko huo ili upate tonge (pellet) la mkaa wa brikiti.
-Inashauriwa ukaushe vizuri kwa kuyaanika juani ili yakauke na kupata brikiti madhubuti.
UBORA WA MKAA BRIKITI
-Unaungua taratibu na kwa masaa 4 zaidi ya mkaa wa kawaida masaa 2.5
-Hautoi moshi
-Una joto madbubuti kwa kuoka
-Bei rahisi
-Unapunguza mkusanyiko wa hewa ya kabon monoksaidi



Jumamosi, 16 Januari 2016

Maelezo ya nembo KUNI AFRIKA (Kutokomeza Umaskini wa Nishati )

Muonekano wa nembo ya KUNI AFRIKA unaelezea athari  za umaskini wa nishati hasa kwa matumizi ya kuni na taa za mafuta ya taa kwa afya ya mama na mtoto jikoni.Shirika la Afya duniani WHO limeeleza uchafuzi wa hewa ndani  ya nyumba hasa jikoni umekuwa chanzo cha vifo vya mama na mtoto takribani milioni 4.3 kwa mwaka kuliko ukimwi,malaria na tb duniani.

Matumizi ya nishati kuni kupikia kwenye jiko la mafiga kuanzia asubuhi mpaka jioni ni sawa na kuvuta pakiti moja ya sigara. Matumizi ya nishati kuni yamekuwa yakichochea umaskini hasa unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke katika kutafuta kuni maporini.Hata kuuwawa kwa imani za kishirikina kutokana na macho yao kuwa mekundu hasa  kupikia nishati duni kama kuni na kinyesi cha ng’ombe jikoni.

Utumiaji wa kuni kama nishati umekuwa ukichangia katika ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu na kuchochea mabadiliko ya tabia nchi.

Kama Kuni Afrika tunajitolea  uelewa wa nishati jadidifu na upatikanaji wa bidhaa zake sokoni kupitia wasambazaji  wa bidhaa rafiki na ikologia Eco Footprints Tz ili kutokomeza umaskini wa nishati. Kuni Afrika ni kampeni ya kuhamasisha kutumia majiko sanifu na nishati mbadala ili kufuatilia Mpango wa upunguzaji hewa ukaa  katika kaya.

Uchomaji uzito uhai na  vichochezi ufu kama vyanzo vya nishati  kunaendeleza  kuharibu mazingira hiyvo hakuna budi kuelimisha jamii kuhusu nishati mbadala kama mkaa endelevu na vifuasi nishati kama jiko lisilotumia moto (fireless cooker),majiko sanifu ya kisasa (modern efficiently stove) kama eco zoom,envirofit,Bio lite cook stove, Cookswell Jiko etc.


Jumatano, 23 Septemba 2015

Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi  wa Misitu Afrika Mashariki

Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga  unachochewa na shughuli  za binadamu hasa uharibifu wa misitu (deforestation) na  kukata miti ovyo (forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama nishati ya kaya.

Utengenezaji  wa mkaa kwa tanuru la udongo usio madhubuti umekuwa chanzo  cha kiwango kikubwa cha hewa ukaa inayopotea katika kitendo cha kukabonisha (carbonization) na kupata mkaa kidogo kulingana na kuni zilizoyotumika. Nchini Kenya kampuni ya siku nyingi ya bidhaa za kuhifadhi nishati Cookswell Jiko wameboresha na  kutengeneza tanuru la pipa la bati kwa kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti ovyo na uharibifu wa misitu.

Tanuru hili la pipa madhubuti  liloboreshwa na kusanifiwa Kenya na wasanii wa Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya nazi,magunzi ya mahindi na mianzi ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha ni mkombozi wa misitu na miti kwa sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa kwa tanuru la udongo, bali kutumia matawi yaliyopogolewa vizuri na kutengeneza mkaa mwenyewe (DIY).

Kwa kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa misitu  na kupunguza hewa ukaa na kufanya Mkaa kuwa Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati kutoka Cookswell Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la kuikarisha (barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book @Cookswell saving jiko.
Tanuru hili la pipa  linapatikana pia Tanzania kwa wasambazaji wa bidhaa rafiki mazingira na nishati jadidifu Eco Footprints Tz na mradi wa kutokomeza umaskini wa nishati KUNI AFRIKA.





                                                         OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU


Jumapili, 13 Septemba 2015

TENGENEZA MWENYEWE BALBU CHUPA YA JUA

Balbu chupa ya  jua ni balbu inayotokana na chupa ya maji  iliyotupwa kama taka kwa kujaza maji pamoja na jiki (bleach)  ili kupata mchanganyiko ndani ya chupa unao pindisha (refraction) miale ya jua. Balbu  chupa ya jua yenye mchanganyiko wa maji na jiki (bleach) , inatakiwa nusu chupa upande wa mdomo kuwa nje ya bati na kitako cha chupa kuwa ndani. Hivyo maji yenye mchanganyiko wa jiki (bleach) hupindisha miale ya jua na kufanya eneo lenye giza kupata mwanga huo wa kati wa mchana hasa katika nyumba za makazi msongamano.

Usanifu huu wa balbu chupa ya jua (solar bottle bulb) umewezesha kupunguza umaskini wa nishati ya mwanga kwa nyumba ambazo hazipati mwanga safi wakati wa mchana kutokana  na kutokuwa na uwezo wa kuunganishiwa umeme wa gridi ya taifa. Usanifu huu umeweza kuwa rahisi kutokana na upatikanaji wa rasilimali hasa chupa zilizotupwa kama uchafu ambazo huchukua zaidi ya miaka  mia tano kuoza hivyo kuzorotesha afya ya mazingira.Pia usanifu huu wa balbu chupa ya umeme jua umesaidia katika mrudisho na matumizi rafiki na mazingira.

MAHITAJI
Chupa ya maji iliyoisha matumizi yake hasa ya lita 1
Jiki (bleach) ya kufulia nguo
Maji safi
Kipande cha bati inchi 9 kwa 10

JINSI YA KUUNGA
Kata mzingo saizi ya kipenyo cha chupa  kwenye kipande cha bati 9 kwa 10
Mzunguko wa mzingo ukatwe vizuri ili kufanya chupa ifiti kwa uthabiti
Kata kipande cha mpira cha saizi ya mzunguko ili kusaidia chupa kushika vizuri ikisaidiwa na gundi.

JINSI YA KUFUNGA
Jaza maji safi kwenye chupa ya lita moja
Weka kiwango cha kifuniko kimoja cha jiki kwenye kwenye chupa ya maji lita moja kupata mchanganyiko wa maji na jiki na funga vizuri kwa kupakalia na gundi.
Baada ya hapo fitisha chupa hiyo ya mchanganyiko kwenye kipande cha bati cha inchi 9 kwa 10 kwa kupakalia gundi ya plastiki pamoja na mzunguko wa kipande cha mpira.
Kata bati la paa ya nyumba saizi ya uwazi mdogo wa 7 kwa 8 ili kupachika kipande cha bati 9 kwa 10 chenye chupa balbu kwenye paa la nyumba.
Paka gundi ya bati upande wa juu pembezoni ya uwazi wa bati 7 kwa 8 ili kufitisha  kipande cha bati cha 8 kwa 10 chenye balbu chupa ya umeme jua
Baada ya hapo utakuwa tayari umefutisha kipande cha bati kwenye paa la nyumba na kuwa tayari kupata mwanga wa balbu jua kupitia chanzo cha nishati ya jua.

FAIDA YA CHUPA BALBU YA UMEME JUA
Balbu chupa ya jua ina uwezo wa kutoa mwanga wa wati 55 wa kati wa mchana jua likiwaka
Rafiki wa mazingira kutokana na mrudisho kwenye matumizi ya chupa tupu ya plastiki baada ya kuisha matumizi yake.


 










Jumatatu, 24 Agosti 2015

Jiko lisilo la moto/Kapu ,begi

Jiko lisilo tumia moto ni jiko linalohifadhi joto na kuendelea kupika chakula kwa mda mrefu kutokana na joto lililohifadhiwa  katika matirio ya kihami (insulate)kwenye ukuta wa kapu au begi.Sufuria ya chakula itapata joto kwenye jiko lolote kabla ya kuhamishiwa kwenye jiko lisilo la moto (kapu au begi).Jiko lisilo la moto si jiko geni katika bidhaa za kifuasi nishati, lipo ila uelewa wa jiko hili ni mdogo hasa katika wateja watumiaji majiko sanifu ya kisasa.
Jiko lisilo la moto ni kifuasi cha majiko aina zote kama jiko la umeme,jiko sanifu la mkaa,jiko la gesi na majiko mengineyo ya yaliyoendelezwa.

Jiko lisilo la moto linajulikana na limekuwwapo kwenye soko katika sehemu mbali mbali barani Afrika mfano  Tanzania linajulikana kama Jiko Kapu wakati Afrika kusini ni maarufu kama begi la ajabu (wonder bag). Jiko hili lisilo la moto limekuwa liki okoa matumizi ya nishati kwa sababu linapunguza matumizi ya nishati hasa kuni na mkaa kwa sababu auhitaji nishati nyingi  kupikia.

Baada ya kupika chakula  kwa kiwango  cha kawaida na  baadaye kuhamishia kwenye sufuria yenye joto kwenye jiko lisilo la moto kufanya chakula kiive taratibu.Epua sufuria ya chakula  ikiwa na joto nakuweka kwenye  kapu jiko  na kufunika na mfuniko vizuri vizuri joto la sufuria lisitoroke.Baada ya hapo chakula kitaendelea kuiva  taratibu kwa kiwango unachotaka kutokana na joto kwenye sufuria kuhamishiwa kwenye ukuta wa kihami (insulate)cha kapu na trei.Jiko hili rafiki wa mazingira linaokoa matumizi mengi ya mkaa na halitoi moshi hivyo ni bora kwa afya ya mtumiaji na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Ni jiko lisilotoa moshi rahisi ambalo ni salama,safi,madhubuti na rafiki wa mazingira linalohifadhi nishati na kusaidia kuhifadhi mazingira. Jiko lisilo la moto linaendelea kupika baada ya sufuria kuondolewa kwenye jiko la kawaida.

Faida
Jiko lisolo la moto lina okoa nishati kwa kutotumia kuni au mkaa mwingi. Jiko hili ni rahisi kutengeneza linahitaji kikapu na malighafi kama nguo kuukuu au material nyingine ambayo ni kihami (insulate) kama majani,mfano sponge zinazo kuja na vifaa vya umeme,
Linapunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 40%
Linapunguza moshi wa ndani (indoor air pollution) hivyo kuokoa afya ya mwanamke na mtoto.

Ni bei rahisi
 Linatumia malighafi ya kawaida na rahisi kutengeneza
Linapunguza matumizi ya maji kupikia kwa asilimia 25%.Maji yana baniwa tofauti na kuchemka,linahifadhi vimea,ladha ya chakula na maji ya kunywa.
Inasaidia kuhifadhi misitu ya asili na mazingira.
Jiko liliso la moto linaweza kutumika kuhifadhia chakula.
Linasaidia wanawake kutengeneza kipato katika fursa nyingine  kwa sababu hatumii muda mrefu kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.

Changamoto
Jiko halijulikani sana na watu wengi hawali tiili maanani

Jamii haina uelewa wa  vyanzo mbadala wa nishati baada ya mkaa na kuni



Jumapili, 17 Mei 2015

Interpretation of DON’T SHOOT BY RIFLE SHOOT BY CAMERA

This is awareness campaign of stop poaching and sensitizes eco-tourism to tourists and local community alike. This awareness show how tourism product made to be consumed by taking pictures and leave nature takes it place. The logo has elephant to show among endangered and extinct who disappear due to wild life crime. The live elephant worth more when shoot by camera than rifle which kill the animal and not sustainable for future generation to meet their need.

 The wild life tourism earned high in the contribution of tourism foreign exchange compare to cultural tourism, wild life tourism contributed by big five wild animal attraction where elephant and rhino are poached heavily. Poaching of elephant and rhino trophy lead to the extinction while the mostly used weapon is rifle followed with local traps. When elephant killed for ivory it disturb ecosystem by killing the key stone species and lead to misbalance of ecological system in protected areas.

To shoot by camera is sustainable way to utilizing tourism products and lead to the sustainable conservation of natural resources. Also don’t shoot by rifle shoot by camera scrutinize hunting tourism which is not in a sustainable way of preserving wild animals and which lead to endanger or extinction of wild animal like elephant and rhino.
The logo also to large extent promotes peace and stop environment crimes and political war which now days engulfing the world.

Photographic tourism is the eco-friendly tourism activities which raises awareness of stop poaching due to the taking picture only and leave animal existence for future generation to see. Also to raise domestic tourism where you can’t see elephant in town what you need is to go in park and see the elephant live and shoot by camera to take memorable nature experience.










                                                                                                    Prepared by Mckene Ngoroma

Jumamosi, 11 Aprili 2015

Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi  wa Misitu nchini Kenya

Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga  unachochewa na shughuli  za binadamu hasa uharibifu wa misitu (deforestation) na  kukata miti ovyo (forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama nishati ya majumbani.Utengenezaji huu wa mkaa kwa tanuru la udongo usio madhubuti umekuwa chanzo  cha kiwango kikubwa cha hewa ukaa inayopotea katika kitendo cha kukabonisha (carbonization) na kupata mkaa kidogo kulingana na kuni zilizoyotumika.

 Nchini Kenya kampuni ya bidhaa za kuhifadhi nishati Cookswell Jiko wameboresha na  kutengeneza tanuru la pipa la bati kwa kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti ovyo na uharibifu wa misitu.Tanuru hili la pipa madhubuti  liloboreshwa na kusanifiwa Kenya na wasanii wa Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya nazi,magunzi ya mahindi na mianzi ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha ni mkombozi wa misitu na miti kwa sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa kwa tanuru la udongo, bali kutumia matawi yaliyobanguliwa vizuri na kutengeneza mkaa mwenyewe (DIY).

Kwa kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa misitu  na kupunguza hewa ukaa na kufanya Mkaa kuwa Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati kutoka Cookswell Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la kuikarisha (barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book na tovuti  yao.

Tanuru hili la pipa  linapatikana Tanzania kupitia Eco Footprints Tz.

Tanuri la pipa la chuma Cookswell Jiko  lililoboreshwa.  OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU



Imeandikwa na Mckene Ngoroma