Translate

Jumatano, 23 Septemba 2015

Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi  wa Misitu Afrika Mashariki

Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga  unachochewa na shughuli  za binadamu hasa uharibifu wa misitu (deforestation) na  kukata miti ovyo (forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama nishati ya kaya.

Utengenezaji  wa mkaa kwa tanuru la udongo usio madhubuti umekuwa chanzo  cha kiwango kikubwa cha hewa ukaa inayopotea katika kitendo cha kukabonisha (carbonization) na kupata mkaa kidogo kulingana na kuni zilizoyotumika. Nchini Kenya kampuni ya siku nyingi ya bidhaa za kuhifadhi nishati Cookswell Jiko wameboresha na  kutengeneza tanuru la pipa la bati kwa kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti ovyo na uharibifu wa misitu.

Tanuru hili la pipa madhubuti  liloboreshwa na kusanifiwa Kenya na wasanii wa Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya nazi,magunzi ya mahindi na mianzi ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha ni mkombozi wa misitu na miti kwa sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa kwa tanuru la udongo, bali kutumia matawi yaliyopogolewa vizuri na kutengeneza mkaa mwenyewe (DIY).

Kwa kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa misitu  na kupunguza hewa ukaa na kufanya Mkaa kuwa Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati kutoka Cookswell Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la kuikarisha (barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book @Cookswell saving jiko.
Tanuru hili la pipa  linapatikana pia Tanzania kwa wasambazaji wa bidhaa rafiki mazingira na nishati jadidifu Eco Footprints Tz na mradi wa kutokomeza umaskini wa nishati KUNI AFRIKA.





                                                         OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU


Jumapili, 13 Septemba 2015

TENGENEZA MWENYEWE BALBU CHUPA YA JUA

Balbu chupa ya  jua ni balbu inayotokana na chupa ya maji  iliyotupwa kama taka kwa kujaza maji pamoja na jiki (bleach)  ili kupata mchanganyiko ndani ya chupa unao pindisha (refraction) miale ya jua. Balbu  chupa ya jua yenye mchanganyiko wa maji na jiki (bleach) , inatakiwa nusu chupa upande wa mdomo kuwa nje ya bati na kitako cha chupa kuwa ndani. Hivyo maji yenye mchanganyiko wa jiki (bleach) hupindisha miale ya jua na kufanya eneo lenye giza kupata mwanga huo wa kati wa mchana hasa katika nyumba za makazi msongamano.

Usanifu huu wa balbu chupa ya jua (solar bottle bulb) umewezesha kupunguza umaskini wa nishati ya mwanga kwa nyumba ambazo hazipati mwanga safi wakati wa mchana kutokana  na kutokuwa na uwezo wa kuunganishiwa umeme wa gridi ya taifa. Usanifu huu umeweza kuwa rahisi kutokana na upatikanaji wa rasilimali hasa chupa zilizotupwa kama uchafu ambazo huchukua zaidi ya miaka  mia tano kuoza hivyo kuzorotesha afya ya mazingira.Pia usanifu huu wa balbu chupa ya umeme jua umesaidia katika mrudisho na matumizi rafiki na mazingira.

MAHITAJI
Chupa ya maji iliyoisha matumizi yake hasa ya lita 1
Jiki (bleach) ya kufulia nguo
Maji safi
Kipande cha bati inchi 9 kwa 10

JINSI YA KUUNGA
Kata mzingo saizi ya kipenyo cha chupa  kwenye kipande cha bati 9 kwa 10
Mzunguko wa mzingo ukatwe vizuri ili kufanya chupa ifiti kwa uthabiti
Kata kipande cha mpira cha saizi ya mzunguko ili kusaidia chupa kushika vizuri ikisaidiwa na gundi.

JINSI YA KUFUNGA
Jaza maji safi kwenye chupa ya lita moja
Weka kiwango cha kifuniko kimoja cha jiki kwenye kwenye chupa ya maji lita moja kupata mchanganyiko wa maji na jiki na funga vizuri kwa kupakalia na gundi.
Baada ya hapo fitisha chupa hiyo ya mchanganyiko kwenye kipande cha bati cha inchi 9 kwa 10 kwa kupakalia gundi ya plastiki pamoja na mzunguko wa kipande cha mpira.
Kata bati la paa ya nyumba saizi ya uwazi mdogo wa 7 kwa 8 ili kupachika kipande cha bati 9 kwa 10 chenye chupa balbu kwenye paa la nyumba.
Paka gundi ya bati upande wa juu pembezoni ya uwazi wa bati 7 kwa 8 ili kufitisha  kipande cha bati cha 8 kwa 10 chenye balbu chupa ya umeme jua
Baada ya hapo utakuwa tayari umefutisha kipande cha bati kwenye paa la nyumba na kuwa tayari kupata mwanga wa balbu jua kupitia chanzo cha nishati ya jua.

FAIDA YA CHUPA BALBU YA UMEME JUA
Balbu chupa ya jua ina uwezo wa kutoa mwanga wa wati 55 wa kati wa mchana jua likiwaka
Rafiki wa mazingira kutokana na mrudisho kwenye matumizi ya chupa tupu ya plastiki baada ya kuisha matumizi yake.


 










Jumatatu, 24 Agosti 2015

Jiko lisilo la moto/Kapu ,begi

Jiko lisilo tumia moto ni jiko linalohifadhi joto na kuendelea kupika chakula kwa mda mrefu kutokana na joto lililohifadhiwa  katika matirio ya kihami (insulate)kwenye ukuta wa kapu au begi.Sufuria ya chakula itapata joto kwenye jiko lolote kabla ya kuhamishiwa kwenye jiko lisilo la moto (kapu au begi).Jiko lisilo la moto si jiko geni katika bidhaa za kifuasi nishati, lipo ila uelewa wa jiko hili ni mdogo hasa katika wateja watumiaji majiko sanifu ya kisasa.
Jiko lisilo la moto ni kifuasi cha majiko aina zote kama jiko la umeme,jiko sanifu la mkaa,jiko la gesi na majiko mengineyo ya yaliyoendelezwa.

Jiko lisilo la moto linajulikana na limekuwwapo kwenye soko katika sehemu mbali mbali barani Afrika mfano  Tanzania linajulikana kama Jiko Kapu wakati Afrika kusini ni maarufu kama begi la ajabu (wonder bag). Jiko hili lisilo la moto limekuwa liki okoa matumizi ya nishati kwa sababu linapunguza matumizi ya nishati hasa kuni na mkaa kwa sababu auhitaji nishati nyingi  kupikia.

Baada ya kupika chakula  kwa kiwango  cha kawaida na  baadaye kuhamishia kwenye sufuria yenye joto kwenye jiko lisilo la moto kufanya chakula kiive taratibu.Epua sufuria ya chakula  ikiwa na joto nakuweka kwenye  kapu jiko  na kufunika na mfuniko vizuri vizuri joto la sufuria lisitoroke.Baada ya hapo chakula kitaendelea kuiva  taratibu kwa kiwango unachotaka kutokana na joto kwenye sufuria kuhamishiwa kwenye ukuta wa kihami (insulate)cha kapu na trei.Jiko hili rafiki wa mazingira linaokoa matumizi mengi ya mkaa na halitoi moshi hivyo ni bora kwa afya ya mtumiaji na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Ni jiko lisilotoa moshi rahisi ambalo ni salama,safi,madhubuti na rafiki wa mazingira linalohifadhi nishati na kusaidia kuhifadhi mazingira. Jiko lisilo la moto linaendelea kupika baada ya sufuria kuondolewa kwenye jiko la kawaida.

Faida
Jiko lisolo la moto lina okoa nishati kwa kutotumia kuni au mkaa mwingi. Jiko hili ni rahisi kutengeneza linahitaji kikapu na malighafi kama nguo kuukuu au material nyingine ambayo ni kihami (insulate) kama majani,mfano sponge zinazo kuja na vifaa vya umeme,
Linapunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 40%
Linapunguza moshi wa ndani (indoor air pollution) hivyo kuokoa afya ya mwanamke na mtoto.

Ni bei rahisi
 Linatumia malighafi ya kawaida na rahisi kutengeneza
Linapunguza matumizi ya maji kupikia kwa asilimia 25%.Maji yana baniwa tofauti na kuchemka,linahifadhi vimea,ladha ya chakula na maji ya kunywa.
Inasaidia kuhifadhi misitu ya asili na mazingira.
Jiko liliso la moto linaweza kutumika kuhifadhia chakula.
Linasaidia wanawake kutengeneza kipato katika fursa nyingine  kwa sababu hatumii muda mrefu kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.

Changamoto
Jiko halijulikani sana na watu wengi hawali tiili maanani

Jamii haina uelewa wa  vyanzo mbadala wa nishati baada ya mkaa na kuni



Jumapili, 17 Mei 2015

Interpretation of DON’T SHOOT BY RIFLE SHOOT BY CAMERA

This is awareness campaign of stop poaching and sensitizes eco-tourism to tourists and local community alike. This awareness show how tourism product made to be consumed by taking pictures and leave nature takes it place. The logo has elephant to show among endangered and extinct who disappear due to wild life crime. The live elephant worth more when shoot by camera than rifle which kill the animal and not sustainable for future generation to meet their need.

 The wild life tourism earned high in the contribution of tourism foreign exchange compare to cultural tourism, wild life tourism contributed by big five wild animal attraction where elephant and rhino are poached heavily. Poaching of elephant and rhino trophy lead to the extinction while the mostly used weapon is rifle followed with local traps. When elephant killed for ivory it disturb ecosystem by killing the key stone species and lead to misbalance of ecological system in protected areas.

To shoot by camera is sustainable way to utilizing tourism products and lead to the sustainable conservation of natural resources. Also don’t shoot by rifle shoot by camera scrutinize hunting tourism which is not in a sustainable way of preserving wild animals and which lead to endanger or extinction of wild animal like elephant and rhino.
The logo also to large extent promotes peace and stop environment crimes and political war which now days engulfing the world.

Photographic tourism is the eco-friendly tourism activities which raises awareness of stop poaching due to the taking picture only and leave animal existence for future generation to see. Also to raise domestic tourism where you can’t see elephant in town what you need is to go in park and see the elephant live and shoot by camera to take memorable nature experience.










                                                                                                    Prepared by Mckene Ngoroma

Jumamosi, 11 Aprili 2015

Tanuru la Pipa la Chuma Cookswell Jiko ni Mkombozi  wa Misitu nchini Kenya

Uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo ni chanzo cha mabadiliko tabia nchi Duniani na uzalishaji wa hewa ukaa kama inavyoainishwa na MKUHUMI (REDDS) .Uzalishaji wa hewa ukaa kwenye anga  unachochewa na shughuli  za binadamu hasa uharibifu wa misitu (deforestation) na  kukata miti ovyo (forest degradation) kwa ajili ya kuanzisha masahamba na kutengeneza mkaa kama nishati ya majumbani.Utengenezaji huu wa mkaa kwa tanuru la udongo usio madhubuti umekuwa chanzo  cha kiwango kikubwa cha hewa ukaa inayopotea katika kitendo cha kukabonisha (carbonization) na kupata mkaa kidogo kulingana na kuni zilizoyotumika.

 Nchini Kenya kampuni ya bidhaa za kuhifadhi nishati Cookswell Jiko wameboresha na  kutengeneza tanuru la pipa la bati kwa kukabonisha matawi ya miti badala ya kukata miti ovyo na uharibifu wa misitu.Tanuru hili la pipa madhubuti  liloboreshwa na kusanifiwa Kenya na wasanii wa Kenya linakabonisha matawi ya miti,mapute ya nazi,magunzi ya mahindi na mianzi ili kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).Tanuru hili bora la kuhamisha ni mkombozi wa misitu na miti kwa sababu hauhitaji kukata miti kutengeneza mkaa kwa tanuru la udongo, bali kutumia matawi yaliyobanguliwa vizuri na kutengeneza mkaa mwenyewe (DIY).

Kwa kutumia tanuru hili la Cookswell Jiko utakuwa umeokoa misitu  na kupunguza hewa ukaa na kufanya Mkaa kuwa Nishati Jadidifu.Ukitaka kujua kuhusu bidhaa za kuhifadhi nishati kutoka Cookswell Jiko pamoja na majiko sanifu (efficiently cookstove),joko la kuikarisha (barbeque oven) na jiko la kuotea tembelea ukurasa wao wa face book na tovuti  yao.

Tanuru hili la pipa  linapatikana Tanzania kupitia Eco Footprints Tz.

Tanuri la pipa la chuma Cookswell Jiko  lililoboreshwa.  OKOA NISHATI: OKOA MISITU YETU



Imeandikwa na Mckene Ngoroma

Jumapili, 5 Aprili 2015

Historia ya Jiko banifu/Sanifu KCJ

Historia ya jiko sanifu barani Afrika inaanzia miaka ya 1970 na kuendelea mpaka miaka ya 1980.Tokea mwaka 1982 Shirika la Nishati na Mazingira Kenya KENGO lilifanya tafiti ikishirikiana na wataalamu wasomi mmojawapo ni Dr Maxwell Kinyanjui kufanya tafiti na kuendeleza matumizi ya jiko la ufinyanzi.Jiko hili lina chimbuko kutoka Thailand ambako lilianzia kutokana na jiko ‘ndoo’.Taasisi kama CARE,UNICEF na Bellerive zimefanya kazi kubwa kutoa mchango wa kifedha na kuwezesha kuendeleza jiko na namna ya kulitengeneza pamoja na mashirika ya misaada kama Marekani (USAID),Ujerumani (GTZ) na mashirika mengineyo. Mtaalamu,msanifu na msomi Dr Maxwell Miringu Kinyanjui kutoka Kenya  alifanikisha maendeleo ya jiko hili kuwa sanifu  na bora kwa matumizi ya nishati ndogo ya mkaa.Kutokana na tafiti,fafanuzi na biashsra ikafanya jiko sanifu  (ufinyanzi) kutambulika kama jiko la kupunguza matumizi  ya nishati ya kupikia mkaa Kenya.Kwa mara ya kwanza jiko kwenda sokoni lilikuwa linauzwa bei ghali kutokana na watumiaji wengi baadhi yao kuwa ni maskini wanaotumia jiko la mafiga matatu. Baada ya kufikiriwa kwa makini hitimisho lilifikiwa na wataalamu kwamba kutokana na jiko ni geni sokoni basi lisi wekewe ruzuku ili liende sokoni lishindane kama bidhaa nyingine na kuleta ushindani thabiti. Mwanzo jiko Sanifu (ufinyanzi) lilikuwa ghali,mauzo yalikuwa taratibu na ubora ulitofautiana kutokana na kuigwa utengenezaji na wasanifu wengine bila kufuata vigezo kuwa na majiko sanifu feki yasiyo na ubora kama ulio kusudiwa.Kuendelea  kuongezeka kwa watengenezaji na wauzaji wa majiko sanifu kukaongeza ushindani na hii ikaongeza uvumbuzi wa kutengeneza chaga za jiko kwa kutumia udongo ufinyanzi pamoja na simenti ili kupata chaga bora itakayo akisi joto na kukaa nalo muda mrefu.

Sehemu ya jiko

Jiko sanifu au jiko banifu lina  chaga ambayo ndio inayobeba mkaa wa moto na kuhifadhi  kutunza kwenye chaga amabayo imetengenezwa kwa udongo wa ufinyanzi ulio na uwezo wakuhifadhi  joto. Hivi sasa  chaga zinaboreshwa kwa  udongo ufinyanzi unachanganywa na simenti  kufanya chaga iwe ngumu na isiharibike mapema.Baadhi ya wasanifu na mafundi majiko wanaoiga jiko hili wamekuwa wakitengeneza chaga zisizo na ubora ulio kusudiwa. Baadhi ya watengenezaji wa majiko haya barani Afrika kama Cookswell Jiko Kenya na Tatedo Tanzania wanashauri chaga  bora ni zile zenye kudumu mda mrefu na uwezo wa kuhifadhi joto lisipotee kuonyesha uendelevu. Jiko hili Sanifu limechangia kukua ujasiriamali  kwa  watengenezaji wa majiko ya kawaida ya bati sasa hivi wanatengeneza  fremu ya jiko na chagga baada ya jiko hili kuwa maarufu katika kaya za Afrika Mashariki.

Kusambaa kuingia Tanzania

Jiko hili sanifu liliingia Tanzania miaka ya 1990 kutokea Kenya pale Shirika la Nishati Asili na Jadidifu Tanzania TATEDO kupata mafunzo kutoka kwa msanifu na muendelezaji  jiko hili barani Afrika Dr Maxwell Kinyanjui. Tatedo walikuwa wa kwanza  kueneza matumizi ya jiko hili na kuwezesha wajasiriamali wa nishati jadidifu ili kutumia jiko hili katika kaya za Tanzania.Mtaalamu wa Cookswell Jiko  Teddy Kinyanjui  anasema ili bidhaa ya jiko sanifu iweze kupenya sokoni inahitaji miaka 10 mpaka 20.Kwa hiyo kwa jiko sanifu (ufinyanzi) KCJ mpaka kufikia mwaka 2002 jiko sanifu lilikuwa limepenya soko la Tanzania na mpaka kufikia mwaka 2012 jiko hili lilikuwa linajulikana na maarufu kama jiko banifu,bora au sanifu. TATEDO wameendelea kupanua aina ya bidhaa hii ya jiko sanifu kwa kutengeneza aina mbalimabali za jiko hili kukidhi  mahitaji ya wateja mbali mbali kama Sazawa.

Faida ya Jiko sanifu

Yana punguza matumizi ya kichochezi nishati (mkaa) kwa asilimi sabini na moja 71%.
Hayachochei  uzalishaji wa moshi hewa ukaa (carbon).
Yana usalama wa joto na bati kutokana na joto kuhifadhiwa katika chaga bila kutorokea kwenye bati
Kumeongeza ajira kwa watengenezaji na ujasiriamali kwa viwanda vidogo vya kutengeneza chaga za ufinyanzi
Yanahifadhi nishati kwenye chaga
Yana dumu muda mrefu
Uzoefu unaonyesha yanapunguza gharama ya matumizi ya mkaa kwa asilimia hamsini 50%
Jiko Sanifu na Mkaa
Jiko hili linategemea mkaa unaotokana na mti ili kuchochea na kuhifadhi joto kwa matumizi ya kupikia.Kumekuwa na dhana potofu kwamba mkaa unatumika na maskini tu na hauna faida yoyote katika jamii au ni ‘nuksi’ katika uhifadhi wa misitu ya asili.Inashauriwa kupanda miti ilikuendelea kupata bidhaa ya mkaa inyotumika katika majiko banifu.Mkaa ni nishati jadidifu kama miti itakuwa inapandwa kwa ajili ya bidhaa mkaa.Pia kila mwananchi kupanda mti katika eneo lake analoishi ili kutengeneza mkaa wake mwenyewe (DIY) kwa kukabonisha  matawi ya miti,magunzi mapute ya nazi na kupata mkaa rafiki mazingira (eco charcoal).

 







Imeandikwa na Mckene Ngoroma kwa msaada wa vyanzo vya taarifa Teddy Kinyanjui  wa  COOKSWELL  JIKO KENYA na TATEDO Tanzania


Alhamisi, 2 Aprili 2015

Eco Footprints Tz ya shiriki kufanya Dar Es Salaam kuwa jiji safi mpaka kufikia 2020

Matembezi na Kuokota WALK &PICK SINZA-TANDALE-MAGOMENI 26 OCTOBA 2014


Tembea na okota ni mpango wa kufanya jiji la  Dar es salaam kuwa safi mpaka kufika  mwaka 2020 (clean Dar by 2020) mpango huu wa kutembea na kuokota taka unfanyika kila jumapili ya mwisho wa mwezi katika mitaa ya jiji la Dar es salaam. Mpango huu ni wakipekee katika aina za matembezi amabayo  nimekuwa nikijitokeza jiini Dar es Salaam. Katika kupinga utupaji taka ovyo wa jamii katika maeneo ya jumuiya na makaazi na kufikia malengo ya kuwa na jiji safi mpaka kufika mwaka 2020 (CLEAN DAR BY 2020). Tembea na okota au walk and pick ni matembezi yaliyoanzishwa na organization inayoitwa Voice Giving iliyoko Kinondoni . 

                               

  Matembezi haya ni ya aina yake  kwa sababu hauhitaji kupiga kelele au kubeba mabango kama ilivyozoeleka ila ni kutembea na kuokota taka taka pembezoni mwa barabara katika mitaa mbalimbali huku ukitoa elimu ya mazingira na kuhifadhi taka.Katika mataembezi haya  jamii  ina elimika ikikuona ukiokota taka kwakujiuliza  masawali mengi , wengine wakikufananisha na waokota  taka plastic kwa ajili ya mrudisho (recycling) wengine wakidhani umepewa pesa kuokota au wengine wakifikiria u wakala kutokana nakuvaa vifaa vya kujikinga. Watu wengine wanadhani  unaokota takataka mtaani kwao wakifikiri ni kisiasa na baadhi ya viongozi wa shinani na kata  wakitaka hata mtu anaejitolea kwa jamii  kama ilivyotokea pale mtaa wa Tandale uzuri eti mpaka uende kwenye ofisi ya kata kupata kibali. Baadhi wanakuliza unfanyia kazi kampuni gani na hii inajihidhirisha kwamba watu wako nyuma kujitolea katika jamii ya kufanya usafi wa mazingira hasa katika makazi yao eti mpaka wafanyiwe au waambiwe  Nipe Fagio. 


Kwa mpango huu uliobuniwa na vijana wa Voice Giving uko sambamba na shindano la WWF Earth Hour City Challeng  ambao umeingiza Dar es Salaam kushindania kuwa jiji safi na kupunguza hewa ukaa kwa kutumia nishati jadidifu na  kupanda miti. Ushirikishi wa jamii katika matatizo yao mfano kutoa elimu kwa wakazi na kuonyesha mfano kwa kufanya usafi wa mazingira na makaazi yetu pamoja na utupaji wa taka za platik sehemu zisizosahihi.Takataka zimekuwa zikizorotesha afya ya mazingira  hasa plastiki ambayo inachukua miaka 1000 kuoza  na kuleta athari mbali mbali katika viumbe hai nchi kavu na baharini.Tembezi  la tarehe 26 octoba  ni tembezi lililonipa changamoto ya kufikiria kwa upana  tatizo na suluhisho la kukabiliana na taka taka katika jiji la Dar es Salaam. Tembea na okota (walk and pick) ni moja ya matembezi ya harakati amabalo nimepata uelewa  na elimu ya kutosha   kama mjasirianali wa mazingira pamoja na kijamii kuhusu taka taka za Dar es salaam.Kuanzia Sinza kijiweni mpaka Shule ya Msingi Magomeni ni elimu niliyoipata katika uchafuzi wa mazingira na tabia za watu wa Dar es salaam katika muono wa taka taka.Kuchelewa kufika kwa halmashauri au watoa huduma ya taka kituoni na kukuta taka zimefurika huku ziki hatarisha afya za wakazi hasa kituo cha pili mtaa wa Tandale uzuri barabarani tulikuta lundo la takataka karibu namazingira wanayo cheza watoto.


Katika tembezi hili takataka nyingi mitaani ni plastic material pamoja na karatasi na maboksi ambayo ni rahisi kurudishwa.Ni baadhi ya maskini wa mijini wanajua habari ya mazingira na kutotupa taka ovyo mfano kuanzia sinza kijiweni mpaka darajani kuingia kata ya Tandale ina taka nyingi zikiwemo plastic za viroba.Mitaro ya maji machafu ndipo taka zilipo tulia ampapo wakazi wanachukulia urahisi huo huku wakisubiri mvua zinyeshe ziweze kusukumiwa  maeneo ya baharini.Taka nyingi ambazo ziko barabarani zinaweza kutokomezwa ikiwa abiria na wenye mabasi kupitia vyama vyao kama DAROBA wata shurutishwa kufuata sharia zilizowekwa tutaweza kutokomeza uchafuzi huu. Sisi wakaazi ndio wazalishaji wa taka taka hasa katika matumizi yetu ya kila siku kufanikisha mahitaji yetu.Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi au kutupa taka sehemu sahihi  baada ya matumizi ya bidhaa zenye vifungashio vya mifuko ya plastiki au kukataa kabisa kufungiwa bidhaa na mifuko ya plastiki. Kila raia awe mhamasishaji wa kutotupa taka ovyo mfano kama mji wa Moshi kila raia anaogopa kutupa taka ovyo kutokana na sherika kali ya kutozwa faini shilingi elefu hamsini
  
hapa managing director wa Eco footprint tz akitembea na kuokota taka

Hapa Md wa Eco Footprints Tz akiongea na watoto kuhusu atahri za uchafu kituo cha pili Tandale
 kufika kituo cha kwanza cha taka taka mtaa wa tandale
Hapa MD wa Eco footprints Tz akitoa elimu ya mazingira 










Jumapili, 8 Februari 2015

IJUE MITI MAARUFU TANZANIA
Ifuatayo ni baadhi ya miti maarufu Tanzania iwe ili pandwa au ilijiotea yenyewe.Baadhi ya miti imekuwa kivutio kutokana na historia na faida yake kwa jamii.Miti ni viumbe hai vinavyojumuisha uzito hai kama ilivyo kwa wanyama na uhai wake ni muhimu kwa dunia endelevu.Miti imechangia katika dhima mbalimbali iwe historia ,elimu,utamaduni,harakati na utalii.Miti ifuatayo ni maarufu kutokana na kuvutia watalii,wasomi na watu wadini na wa matambiko kutoka maeneo tofauti Tanzania na dunia kwa ujumla.
Mdegree Tree (FICUS)
Mti huu unapatikana katika chuo kikuu cha Dar es Salaam ni mti maarufu uliopandwa mwaka 1960 na raisi wa kwanza wa Tanzania Mwl J.‪#‎Nyerere‬.Mti huu ulioko mbele ya ukumbi wa Nkuruma hall unaopatia wanafunzi kivuli cha kusoma na kupata degree zao.Mahali pa mti huu ndipo harakati za maandamano na migomo ya wanafunzi huanzia.Mahali hapa pa mti huu pana mazingira mazuri ya kusomea pamoja na mtandao wa bure.

Mwembe waliokutana Dr David Livingstone na Stanley
Mwembe huu ulioko ‪#‎Ujiji‬ ‪#‎Kigoma‬ karibu na jumba la makumbusho la ‪#‎Dr‬Livingstone ndipo walipokutana wachunguzi karne ya 19.Mwembe huu uko chini ya idara ya Mali kale kama kumbukumbu ya historia ya bara.Mwembe huu mpaka leo umesimama na kuvutia watu mbalimbali duniani.

Afbeeldingen van Kigoma – vakantiefoto’s










Mbuyu wa kujificha Majangili (poachers hide)
Mti huu aina ya mbuyu(Adansonia digitata) unapatikana katika hifadhi ya taifa Tarangire.Hapo zamani mbuyu huu ulikuwa unatumika pango la kujificha majangili waliokuwa wanawinda wanyamapori ndani ya hifadhi.Mbuyu huu katikati unapango ambalo wanaweza kuingia takribani watu arobaini.Mbuyu huu unavutia watalii wanaotembelea hifadhi ya ‪#‎Tarangire‬ na ni mojawapo ya rasilimali ya utalii inayopatikana katika hifadhi ya Tarangire.2982398831_2b5a4ecb70_z.jpg

Mbuyu wa kanisa
Mti huu ni maarufu na muhimu kwa kanisa katoliki na historia yake ya kuenea kwa ukiristo Afrika Mashariki.Mbuyu huu unaopatikana katika mji mkongwe wa‪#‎Bagamoyo‬ ulipandwa mwaka 1860 na padri Anthony Horner kwa misheni ya Katoliki Bagamoyo.Mti huu jinsi unavyokuwa kwa Wakatoliki ndo jinsi imani ya Kanisa Katoliki linavyoenea Afrika Mashariki.Mti huu una baki ya mjororo uliokuwa unatumika kufunga punda wa muuguzi Madame de Chevalier mnamo mwaka 1895.






















Mvule wa Ajabu
Mvule wa Ajabu ni mti maarufu unaopatikana katika hifadhi ya msitu wa Rau‪#‎Moshi‬ inasemekana na Tanzania Tourist Board kwamba ndo mvule wenye umri mrefu ‪#‎Afrika‬.Mti huu wenye umri takribani miaka 194 umeweza kudumu umri huu katikati ya miti mingi muhimu ya mbao na sgughuli za binadamu kutokana na mila na desturi za wananchi wanaozunguka msitu huu.Historia inayo kwamba mti huu ulikuwa ukikatwa unatoa damu pamoja na shughuli za matambiko mti huu ukapona na kutimiza umri mrefu kati ya miti ya mivule Tanzania.Hii inaonyesha kwamba mila na desturi zetu za Mwafrika zilikuwa zinasaidia kuhifadhi mimea na wanyama toka kale.Mti huu ni rasilimali ya utalii katika ‪#‎Msitu‬ wa Hifadhi Rau.ndio maana Rau Rau eco and cultural tourism programme wanaendeleza mpango wao mahsusi wa utalii ikiwa kivutio kikubwa ni Mvule wa Ajabu.
Hii ni baadhi ya miti maarufu michache inayopatikana ‪#‎Tanzania‬ na ipo katika uhifadhi uwe wa Mali Asili au Mali Kale.Makala ni maalumu kwa kutambua michango miti katika historia,tamaduni na maisha yetu ya kila siku.
Imeandikwa na mkumbatia Mti Mckene Ngoroma ‪#‎TREEHUGGER‬

Jumamosi, 7 Februari 2015

Kutokomeza Umaskini wa Nishati Afrika

Kutokomeza Umasikini wa Nishati (KUNI) AFRIKA,
Ni mpango wa Eco Footprints Tz wa kujitolea na kuwezesha jamii kutokomeza umaskini wa nishati kupitia uelewa wa rasilimali endelevu pamoja na matumizi ya nishati jadidifu na kuhifadhi mazingira.
Mpango huu una mkakati wa kujitolea katika elimu, vitumizi na vichochezi vya nishati jadidifu  mfano  balbu jua,mkaa endelevu,majiko sanifu katika maeneo ambayo yameathirika na mabadiliko tabia nchi kutokana na ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu.Aidha baadhi ya maeneo hayo  yamepata elimu na uelewa kutoka mashirika mbali mbali kwa hiyo kujitolea katika maeneo haya ambayo yana umuhimu katika nchi kiekologia na haki za binadamu.

 Mfano Barafu iliyoko mlima Kilimanjaro inaendelea kuyeyuka na hii inachangiwa kimataifa na kitaifa kwa hiyo tukiwa kama wa ndani tunaona ni mchango wetu kushiriki “Kutokomeza Umaskini wa Nishati”KUNI ambayo inaleta mabadiliko tabia nchi na kuathiri haki za binadamu, jinsia pamoja na vyanzo vya vifo. Matumizi ya nishati hai ni endelevu kama itafuatiliwa na kuwa rasmi tutaendelea kushi na amani na asilia yetu.Tuna mpango wa kujitolea usanifu wa bidhaa rafiki mazingira pamoja na majiko sanifu,taa za solar na kutoa elimu ya kutengeneza vichochezi hai , kuongeza wigo mpana wa upatikanaji wa bidhaa  sokoni na kama chanzo cha mapato kwa kaya.

 Kutokana na kuvumbuliwa kwa mafuta na gesi Afrika mashariki hii inaleta kushiriki katika mchakato huu ili kuleta kufaidika kwa jamii na maendeleo endelevu na biashara ya  hewa ukaa inayotokana na kuvuna nishati ufu  na hii kwa upande mwingine inatakiwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Biashara ya nishati enedelevu  inafaa kunufaisha jamii kupitia ujasiriamali wakuzalisha na kusambaza  bidhaa za nishati jua .

Kutokana na  ‘kufufua’ nishati ufu na kuhatarisha maisha ya viumbe hai nishati jadidifu ndio mkombozi wa baadae.Hivyo basi inchi za Afrika  yaani Kenya,Tanzania Uganda,Mozambique na Angola zitatokomezaje umasikini wa nishati  kupitia  mkongo off gird  na huku ikipunguza uzalishaji wa gesi joto kutokana na nishati ufu.

Mpango KUNI Afrika unafanya tathmini kwenye kila kaya inayojitolea vifaa tumizi nishati jadidifu hasa katika maeneo yaliyoathirika na ukataji na uharibifu wa misitu na umaskini wa nishati.Katika hili wanatumia ufuatiliaji wa upunguzaji hewa ukaa katika kaya kwa lugha ya kingereza indoor air pollution IAP.

”Biomass will remain the major source of energy for rural populations, coupled with niche renewables such as Solar PV, provided they are affordable, reliable and a proper payments system is established9”  Evance Kitui